November 15, 2015

Athari ya Boko Haram

Na David Wafula

 mapema hii, taifa lenye idadi kubwa zaidi Afrika, Nigeria iliapisha mawaziri wake wapya, Moja ya

changamoto kubwa ambayo Rais Mohammadu Buhari itakuwa vita dhidi ya Boko Haram,

changamoto ambayo ameapa kuimaliza ifikapo mwishoni mwa mwaka huu. Kundi hili la wapiganaji

linashutumiwa kutekeleza maelfu ya maafa na kusababisha watu zaidi ya millioni mbili kukimbia

makwao. "tuliamshwa na milio ya risasi, kwanza nilidhani ni majeshi labda wanajaribu silaha zao,

punde niligundua kwamba ni makabiliano, nilijawa na hofu, kila mtu alizama katika harakati za

mguu niponye, familia ilisambaratishwa, kwa masiku tulitembea vichakani, wengine tulibahatika

kupata maji na maziwa kutoka kwa wachungaji wa mifugo, wanawake na watoto walipata lishe ya

matunda, wakati tu tilitia nanga mjini nikagundua kwamba baba yangu aliuawa" mohammed

anataurifu hii hapa taarifa zaidi....




Mwanamke anayetetea walio na virusi vya Ukimwi

Na David Wafula

 14 Oktoba 2015

 Phindile Sithole-Spong ni mwanaharakati kutoka Afrika Kusini anayeishi na virusi vya Ukimwi.

Amekuwa akiongoza juhudi za kukabiliana na unyanyapaa dhidi ya watu wanaoishi na virusi vya

Ukimwi na hususan miongoni mwa vijana. taarifa hii inayosimuliwa na David Wafula.



Jeshi la Kenya latuhumiwa Somalia

Na David Wafula

12 Novemba 2015

 Jeshi la Kenya limetuhumiwa kujihusisha na biashara, badala ya kufanya kazi zinazowahusu nchini

Somalia. Taasisi ya Wanahabari Wanaopigania haki imelituhumu jeshi hilo kujiingiza katika masuala

yanayowaletea faida. Taasisi hiyo imewalaumu baadhi ya maofisa wa jeshi kushirikiana katika

biashara haramu na wapiganaji wa Al Shabaab. Sikiliza mahojiano ya David Wafula na Msemaji wa


Jeshi la Kenya Kanali David Obonyo, ambaye anakanusha tuhuma hizo