February 9, 2014

HABARI

Moto Saudi Arabia


Watu wasiopungua 15 wamepoteza maisha na wengine 130 kujeruhiwa baada ya hoteli moja kuteketea moto katika mji mtakatifu wa madina nchini Saudi Arabia.
Vyombo vya habari vya saudia vimesema hoteli hiyo ilikuwa na wageni 700 ambao walikuwa mjini madina kwa ajili ya ibada ya umrah. Moto huo ulianza ijumaa usiku na kuendelea hadi mapema jumamosi.

Onyo kwa wakuu wa  Shule
 
Rais Uhuru Kenyatta ametoa onyo kwa wakuu wa shule za umma dhidi ya kuongeza karo akisema kuwa hatua hiyo ni kinyume cha sheria na inafaa kusitishwa mara moja.
Rais Kenyatta amewataka wakuu wa shule kutotoza wazazi fedha zaidi ya kile kinachohitajika na kunyima wanafunzi haki ya kupata elimu.