Moto Saudi Arabia
Watu wasiopungua 15 wamepoteza maisha na wengine 130 kujeruhiwa baada ya hoteli moja kuteketea moto katika mji mtakatifu wa madina nchini Saudi Arabia.
Vyombo vya
habari vya saudia vimesema hoteli hiyo ilikuwa na wageni 700 ambao walikuwa
mjini madina kwa ajili ya ibada ya umrah. Moto huo ulianza ijumaa usiku na
kuendelea hadi mapema jumamosi.
Onyo kwa wakuu wa Shule
Rais Uhuru Kenyatta ametoa onyo kwa wakuu wa shule za umma dhidi ya kuongeza karo akisema
kuwa hatua hiyo ni kinyume cha sheria na inafaa kusitishwa mara moja.
Rais Kenyatta
amewataka wakuu wa shule kutotoza wazazi fedha zaidi ya kile kinachohitajika na
kunyima wanafunzi haki ya kupata elimu.


No comments:
Post a Comment