November 5, 2015

Dj Creme Del Creme Apologizes Over Sex Tape

Diana Busolo                              Entertainment News 
photo courtesy of mirror website






















Creme Del Creme a well known Dj in Kenya apologizes for his sex tape that went viral which involved an intimate time with a socialite by the name Halima.
He wrote: “My guilt is beyond doubt. My shame is enormous. I admit my wrong and take full responsibility for it.”
Saying sorry to his children but not directly his wife he said: “To my family, I truly I am sorry. You are my rock,the foundation upon which I find strength. I apologize for bringing shame to our trust, your names, persons' and legacy.
The tape had been shot  in 2011 and happen to be shopped before being leaked online.



https://soundcloud.com/dee-kandy/vivi-finale



WAIGURU HANGATUKI NG`O




By Crane Senteman
Waziri wa ugatuzi na mipango maalum Bi. Ann Waiguru amesema kuwa hatongatuka uadhifa wake kama waziri kutokana na kile anachosema kuwa yeye si mfisadi,lawama hiyo sasa akiwawekea wakuu wa fedha katika sekta hiyo muhimu.Yakijiri hayo mbunge wa nandi hills alfred keterr ameendelea kutafuta sahihi zitakazotosha kumngatua Waiguru kwenye cheo hicho akidai kuwa anapaswa kuondoka na kufuata mkondo wa mawaziri waliotangulia ili ufanyike uchunguzi.

Chelsea wampunguzia presha Mourinho

Sharon Kutto
Mourinho
Picha kwa hisani ya Supersport

Chelsea walimpunguzia presha meneja wao Jose Mourinho baada ya bao la dakika za mwisho kutoka kwa Willian kuwapa ushindi muhimu wa 2-1 katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Dynamo Kiev uwanjani Stamford Bridge.
Mourinho amekuwa na masaibu mengi, baada ya klabu yake kuanza vibaya sana kampeni ya kutetea taji la Ligi ya Premia, kwa sasa wakiwa nambari 15 kwenye jedwali.
Ilionekana kana kwamba matatizo yao yangezidi baada ya Aleksandar Dragovic kufidia bao lake la kujifunga kwa kutumia vyema kosa la kipa Asmir Begovic na kufungia timu yake bao la kusawazisha mechi ikiwa imesalia dakika 13 kumalizika.
Mashabiki wa Chelsea, walioimba jina la Mourinho mechi yote, lazima waliingiza maji tumboni lakini Willian aliwaokoa kwa kombora kali alilolitoa akiwa hatua 25 kutoka kwenye goli dakika sita baadaye.

Ushindi huo ulifikisha Blues nambari mbili Kundi G, wakiwa alama tatu nyuma ya viongozi Porto lakini sasa wana pengo la alama mbili kati yao na Dynamo Kiev. Mourinho alihitaji sana kitulizo na alikuwa na furaha mashabiki walimuunga mkono.

Huduma za Safaricom za Mpesa Kuimarishwa

Leah Wanjiru














 
Photo courtesy of Safaricom

https://soundcloud.com/user-576496317/leah-voice

Kampuni ya mawasiliano ya Safaricom imeshirikiana na benki nane humu nchini kuimarisha huduma zake za lipa na M-pesa.Mpango huo utawawezesha wateja wa Safaricom kuweka pesa zao kwenye akaunti ya benki moja kwa moja kutoa kwenye vituo vya  lipa na M-pesa hadi akaunti zao za benki,hili ikiwa ongezeko kutoka shilingi milioni tano.

Afisa mtendaji wa Safaricom Bob Collymore amesema ushirikiano huo utapunguza muda wa kuhamisha fedha chini ya mpango huo.
Benki ambazo zimetia saini mkataba huo ni KCB,Equity,Jamii Bora,Chase Bank,Cooperative,Diamond Trust na ile ya Consolidated.


Yaya Toure awania taji ya mchezaji bora

Sharon Kutto

Yaya Touré
Picha kwa hisani ya Supersport

Yaya Toure awania taji la mchezaji bora kutoka barani Afrika kwa mara ya tano, huku Wanyama akichujwa.Kiungo wa kati kutoka Kenya anayecheza soka ya kulipwa na klabu ya Uingereza ya Southampton, Victor Mugubi Wanyama, amechujwa tena kwa kinyang`anyiro cha kuwania taji la mchezaji bora wa Afrika mwaka huu. Hii ni baada ya jina lake kukosekana kwa orodha ya mwisho iliyotolewa.
Wanyama alikuwa kati ya wachezaji 37 waliokuwa wameorodheshwa kuwania taji hilo mwaka huu lakini hakufanikiwa kuingia katika kumi bora. Anayepigiwa mpato sana kulitwaa taji hili ni mshindi mtetezi Yaya Toure anayesakata soka na klabu ya Manchester City na pia ndiye nahodha wa timu ya taifa ya Ivory Coast. Mpinzani wake mkuu ni mshambulizi wa Borussia Dortmund na timu ya taifa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang.