November 5, 2015

Yaya Toure awania taji ya mchezaji bora

Sharon Kutto

Yaya Touré
Picha kwa hisani ya Supersport

Yaya Toure awania taji la mchezaji bora kutoka barani Afrika kwa mara ya tano, huku Wanyama akichujwa.Kiungo wa kati kutoka Kenya anayecheza soka ya kulipwa na klabu ya Uingereza ya Southampton, Victor Mugubi Wanyama, amechujwa tena kwa kinyang`anyiro cha kuwania taji la mchezaji bora wa Afrika mwaka huu. Hii ni baada ya jina lake kukosekana kwa orodha ya mwisho iliyotolewa.
Wanyama alikuwa kati ya wachezaji 37 waliokuwa wameorodheshwa kuwania taji hilo mwaka huu lakini hakufanikiwa kuingia katika kumi bora. Anayepigiwa mpato sana kulitwaa taji hili ni mshindi mtetezi Yaya Toure anayesakata soka na klabu ya Manchester City na pia ndiye nahodha wa timu ya taifa ya Ivory Coast. Mpinzani wake mkuu ni mshambulizi wa Borussia Dortmund na timu ya taifa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang.

No comments: