Irene Ngina 2/12/2015
Alex (katikati)
Picha kwa hisani ya wikipedia
Mtoto alex
ambaye ni mmoja wa watoto wanaounda kundi la “Ghetto kids” ambao wanafanya kazi
na msanii toka uganda Eddy Kenzo, amefariki dunia huku mwingine kwa jina Patricia
yuko hali mbaya baada ya kupata ajali ya baiskeli.
Kwa mujibu wa
William Mashal ambaye ni mmoja wa watu wao wa karibu sana amesema kwamba wawili
hao walikuwa wakiendesha baiskeli ambayo ilikatika breki na kutumbukia mtaroni.
Eddy Kenzo ametangaza kifo cha Alex jumatatu usiku huko Kampala Uganda.
Alex na Patricia walikuwa miongoni mwa “Ghetto kids”
ambao walijipatia umaharufu duniani baada ya kucheza video ya wimbo wa Sityalos
wa Eddy Kenzo na kuwa miongoni ya video zilizotazamwa ulimwenguni kote.
https://soundcloud.com/eyereen-931981221/kifo-mp3

No comments:
Post a Comment