WAIGURU AHOJIWA NA EACC
Waziri wa Ugatuzi na Mipango ya Taifa Anne Waiguru
yuko katika makao makuu ya Tume ya Maadili na Kukabili Ufisadi, EACC.Waiguru
amewasili katika ofisi za EACC akiwa ameandamana na Wakili wake Ahmed Nassir
Abdulahi. Kiongozi huyo anatarajiwa kuhojiwa kuhusu madai ya ufisadi
katika wizara yake pamoja na shutma za kutoajibikia ofisi yake,Kuhojiwa kwake
kunajiri wakati mamia ya vijana waliobebea mabango kumsifu Waiguru wakiandamana
nje ya ofisi ya EACC.Masaibu ya Waiguru yalianza mwezi Juni wakati uchunguzi
ulipobaini kuwa shilingi milioni mia saba tisini na moja ziliporwa na sheria za
ununuzi wa mali ya umma kukiukwa katika Taasisi ya Huduma kwa Vijana, NYS.
BY CRANE SENTEMAN.

No comments:
Post a Comment