December 2, 2015

Uchunguzi Wa Bundi Ya Euro



Fridah Nyanchama                                                        2/12/2015












Mkuu wa mashtaka Keriako Tobiko amewaangiza maafisa wa polisi na idara za kubambana na ufisadi kuchunguza madai ya ufisadi kuhusu uuzaji wa bundi za euro na kuwasisirisha ripoti kwa muda wa siku kumi. Tobiko amesema maafisa hao wanafaa kutadhimini stakabadhi muhimu na kuwasilisha ushahidi kuhusu madai yanayoibuliwa, haya yamejiri wakati wizara ya fedha ikisema muungano wa code una uhuru wa kuchunguza jinsi fedha zilizotokana na uuzaji wa bundi ya euro zilivyo tumika. Waziri Henry Rotiich amesema kwamba wizara hio imemwalika kinara wa Code Raila Odinga kwenye ofisi zake Ijumaa saa nne asubuhi ili kuchukua stakabadhi kisha kuzichunguzaViongozi wa muungano wa Cord, walimtaka Rais Uhuru Kenyatta kuacha hasira serikali yake inapotakiwa kujibu maswali kuhusu kashfa za ufisadi.
Walisema kwamba wako tayari kutoboa mengi zaidi kuhusu kashfa za ufisadi serikalini na hasa pesa za mkopo wa dhamana wa Euro zilivyoporwa.“ Bw Rais hasira ni hasara. Meza hasira yako na uoongoze vita dhidi ya ufisadi ambao  ndio unatatiza serikal yako.” Alisema kiongozi wa Cord Raila Odinga.


 https://soundcloud.com/eyereen-931981221/02codemp3

No comments: