November 6, 2015

Makwatta Afurahi kuvunja Rekodi

 Sharon Kutto
Image result for ulinzi stars
Picha kwa hisani ya ulinzistars.com
https://soundcloud.com/shaz-kutto/spoti
Mshambulizi wa Ulinzi Stars John Mark Makwatta amevunja rokodi yake mwenyewe ya ufungaji wa mabao hata kama hakufanikiwa kufikia lengo lake la kufunga bao 15 katika ligi kuu ya Premia KPL msimu huu.
Makwatta alimaliza msimu akiwa mhezaji bora katika klabu yake, na wa tatu katika kinyang`anyiro cha kiatu cha dhahabu (Golden Boot), akiwa nyuma ya mshindi Jesse Were na Michael Olunga huku Were akiwa amefunga bao 22 naye Olunga bao 19.
Akiongea kupitia tovuti ya klabu yake, Makwatta alisema kuwa alifurahia mchezo wake msimu huu, na kuongeza kuwa iwapo watatwaa taji la Shield Tournament, itakuwa njia bora ya kukamilisha msimu.

No comments: