Mashirika ya USAID na lile la Taifa la Kusambaza Dawa Nchini, KEMSA, yametia saini mkataba wa shilingi bilioni sitini na tano, fedha za kusambaza dawa na vifaa vya matibabu.
Akihutubu katika hafla ya kutia saini mkataba huo, Balozi wa Marekani nchini Robert Godec amesema watafuatilia kwa makini utumizi wa fedha hizo ili kuzuia ufujaji.
Ikumbukwe kuwa serikali ya Marekani imekuwa ikifadhili KEMSA kwa kipindi cha miaka kumi na mitatu sasa, kutoa dawa za kuyatibu magonjwa mbalimbali zikiwamo dawa za kupunguza makali ya virusi vinavyosababisha ukimwi.
By crane senteman

No comments:
Post a Comment