November 27, 2015

Faida za Standard Chatred

 Leah Wanjiru


 Benki ya standard chartered imetangaza faida zake za robo ya tatu japo faida hizo zimeonekana kupungua kwa asilimai 21.4 na kufikia shiingi bilioni 8.7
Mapato ya hisa pia yamepungua kwa asilimia 25.8 huku hisa moja ikiuzwa kwa shilingi 19.57 kiwango cha chini kuliko kipindi sawia na hicho mwaka janai ilipouzwa shilingi 26.32

Katika taarifa zingine za biashara,Kampuni ya ujenzi wa nyumba  ya Stanlip Fahari ni miongoni mwa kampuni zinazouza hisa zao za kwanza leo huku shughuli za uuzaji hisa katika soko la Nairobi zikirejelewa leo.Stanlip ndio kampuni ya kwanza ya ujenzi wa nyumba kuwekwa katika soko hilo.Afisa mtendaji Antony Mulkman ameelezea matumaini ya kuongezeka kwa mapato  yake kufuatia hatua hiyo.

No comments: