Leah Wanjiru Biashara 19 10 2015
Shirika la posta limetia saini mkataba wa ushirikiano na duka la kuuza bidhaa kupitia mtandao la Kil Mall ili kuwezesha wateja wa Kil Mall kupata bidhaa wanazonunua kupitia vituo vya posta kote nchini.
Wateja hao pia wataweza kuagiza bidhaa wanazotaka kununua kupitia matawi ya posta.Afisa mkuu wa posta Enock Kinaro amesema hatua hiyo itaondoa changamoto ya kupta bidhaa kwa wateja walio katika maeneo ya mbali.
Meneja wa Kil Mall Bracil Nyaga amesema hatua hii itawasaidia kufikia wateja zaidi.
# # #
No comments:
Post a Comment